-->

AL QUR-AAN

Kauli Za Salaf Qur-aan

Imaam Adhw-Dhwahaak (Rahimahu Allaah) amesema: "Itafika zama ambapo watu watatundika misahafu kiasi cha kutandwa na buibui na watu hawafaidiki nayo." [Jami’ Bayaanul ‘Ilm (3/271)]

SUNNAH

Kauli Za Salaf Sunnah

Jifunzeni Sunnah Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Zifanyieni Kazi Ni Shifaa Na Sharaf Yenu

TAWHIYD

Kauli Za Salaf: 'Aqiydah-Tawhiyd

Jambo Tukufu Kabisa Ni 'Ilmu Ya Tawhiyd

‘Ilmu-Da’wah

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: Itambulishe (ifundishe) Sunnah wala usiifanyie magomvi.” [Al-Aadaab Ash-Shar-‘iyyah li-ibn Muflih]

Manhaj

“Allaah Amrehemu mja aliyesema haki na akafuata athar (nyayo za Salaf), akashikamana na Sunnah, na akafuata mfano wa wema, na akajiweka pembeni na watu wa bid’ah na akaacha vikao vyao kwa kutaraji malipo na kutaka kujikurubisha kwa Allaah.”

Taqwa-Ikhlaasw

“Ikhlaasw kwa Allaah (Kumsafishia niyyah) ni msingi wa Dini na ni kiini cha Tawhiyd na ‘ibaadah. Nayo ni mja kukusudia ‘amali zake zote kwa ajili ya kutafua radhi za Allaah na thawabu Zake na Fadhila Zake.

Karibu Kutub As-Sunnah كُتُبْ السُّنَّة

Karibu katika blog yetu ya Kutub As-Sunnah كُتُبْ السُّنَّة hapa tunakuletea mkusanyiko wa Ahadiyth zote kwa mtiririko wa vitabu kamili ambavyo tutakuwa tunavitafsiri

Buluwgh Al-Maraam بُلوغ الْمَرام

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn رِياض الصّالِحين

Swahiyh Al-Bukhaariy صحيح البخاري

Jaami' At-Tirmidhiy جامع الترمذي

Kitaongezwa hivi karibuni

Kitaongezwa hivi Karibuni

Progress History

Progressively maintain extensive infomediaries via extensible niches. Dramatically disseminate standardized metrics after resource-leveling processes

Al Qur-aan
90%
Al Hadiyth
75%
Siyrah & Historical
85%
Lugha
55%

WHAT PEOPLE Says

Mashaallaah ni tovuti nzuri na tunashukuru munatuwekea vitu vyenye manufaa na ummah wetu Allaah awalipe kheyr na awaondoshee madhila katika harakati zenu.

Abu Ghufairah

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In ultrices, elit sed faucibus pharetra, diam mauris bibendum orci, sit amet ullamcorper purus dui sit amet augue. Donec aliquet diam ut neque mattis, eu tristique sem rutrum.

Renata Martis

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In ultrices, elit sed faucibus pharetra, diam mauris bibendum orci, sit amet ullamcorper purus dui sit amet augue. Donec aliquet diam ut neque mattis, eu tristique sem rutrum.

Jhon Kwick

Happy Clients

Expert Workers

Projects Done

Years Of Experience

LATEST NEWS

Hapa chini tunakuwekea makala mpya zinazopatikana katika blog.

Tuesday 21 December 2021

Maana Ya Hadiyth Dhwa'iyf

Maana Ya Hadiyth Dhwa'iyf

 


‘Ulamaa wanasema kuwa Hadiyth Dhwa’iyf (dhaifu) ni ile isiyokuwa na sifa zinazokubalika. Na wengine wakasema kuwa Hadiyth Dhwa’iyf ni ile isiyostahiki kuitwa Sahihi wala Hasan.

Zipo aina nyingi ya Hadiyth Dhwa’iyf zikiwemo:

 

 

Mursal:

 

Nazo ni zile zilizonyanyuliwa moja kwa moja kutoka kwa Taabi'iy mpaka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Taabi'iy ni Muislamu aliyeishi wakati wa  Swahaba  akawaona lakini hajamuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Kwa mfano Taabi'iy aseme:

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema…

 

Wakati yeye hajawahi kuonana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

‘Ulamaa  wamekhitalifiana katika makundi manne juu ya kuzitumia Hadiyth za aina hii:

 

 

1-Imaam Abu Haniyfah na Imaam Maalik na baadhi ya Wanazuoni wanasema kuwa Hadiyth hizi zinafaa kutumika.

 

2-Imaam An-Nawawiy akieleza juu ya Jamhuwr kubwa ya ‘Ulamaa na pia akimnukuu Imaam Ash-Shaafi'iy anasema kuwa Hadiyth za aina hii zinaweza kutumika kama ni hoja lakini si hoja ya moja kwa moja (ya kutegemewa).

 

3-Imaam Muslim anasema: “Hadiyth Mursal kwetu sisi na kwa wengi kati ya wanavyuoni si hoja hata kidogo.”

 

4-Wengine wakasema kuwa inaweza kuwa hoja pale tu ikiwa imepokelewa kutoka kwa Taabi'iy mkubwa, kisha Hadiyth hiyo iwe imefanyiwa kazi na Swahaba yeyote au na Wanazuoni wengi.

 

 

Munqatwi'i:

 

Hizi ni zile Hadiyth zilizokatika Isnaad zake, kukatika huko ni sawa kuwe mwanzo au mwisho wa majina ya wapokezi.

 

 

Al-Mudallas:

 

Nazo ni zile Hadiyth ambazo muelezaji aeleze kuwa amehadithiwa na mtu aliyeishi katika zama moja kisha ikathibiti kuwa hawajapata kuonana. Au ahadithie kama kwamba amehadithiwa na mtu huyo wakati ukweli ni kuwa hakuhadithiwa na mtu huyo, kwa mfano aseme:

 

“Amenihadithia fulani.” Au: “Nilimsikia fulani.” Wakati ingekuwa sahihi kama angesema:

“Amesema fulani.” Au: “Kutoka kwa fulani.”

 

‘Ulamaa wanasema kuwa Mudallis (muelezaji wa Hadiyth hizi) hazikubaliwi Riwaayah zake hata kama aliwahi mara moja tu katika maisha yake kusema uongo katika Hadiyth.

 

Wengine akiwemo Imaam Ash-Shaafi'iy wakasema kuwa: “Ni zile Hadiyth alizodallis tu hazikubaliki, lakini zile alizozielezea kwa njia Swahiyh zinakubalika.”

 

 

Mudhwtwarib:

 

Nazo ni zile Hadiyth nyingi zinazogongana. Hadiyth aina hii zimedhoofishwa kwa sababu ya kugongana kwake na kutokuwa thaabit.

 

 

Munkar:

 

Nazo ni zile zilizohadithiwa na ‘Dhaifu’ (mtu asiyeaminika) kisha zikakhitilafiana na Hadiyth zilizohadithiwa na Thiqqah (mtu mwenye kuaminika).

 

 

Al-Mudhwa'af:

 

Nazo ni zile Hadiyth zilizodhoofishwa na baadhi ya ‘Ulamaa kutokana na udhaifu wa wapokezi wake, wakati baadhi nyingine ya ‘Ulamaa wakasema kuwa ni Swahiyh.

 

 

Al-Matruwk:

 

Nazo ni zile zilizohadithiwa na mtu anayetuhumiwa kwa uongo katika Hadiyth au hata katika mazungumzo yake. Au anayetuhumiwa kuwa ni Faasiq (fasiki) wa maneno au vitendo. Matruwk pia ni yule mwenye kusahau sana au mwenye kukosea sana.

 

 

Wakati Gani Hadiyth Dhwa’iyf Inakuwa Na Nguvu?

 

Hadiyth dhaifu inapata nguvu pale tu ikiwa Raawiy wake (mwenye kuhadithia) anatuhumiwa kuwa ameanza kusahau sahau. Ni Sharti awe Thiqqah hatuhumiwi kwa Uongo wala kwa ufasiki wala kwa kusahau sana. Kisha Hadiyth alozungumza juu yake ziwe zimepokelewa kwa njia nyingi sana, na hapo inapanda daraja na kuwa ‘Hadiyth Hasan.’

 

Na hii ni kwa sababu imepokelewa kwa njia zinazokubalika tena kwa njia ya Raawiy asiyetuhumiwa kwa uongo au kwa sababu ovu za kumdhoofisha.

 

 

Kuzifanyia Kazi Hadiyth Dhaifu:

 

‘Ulamaa wamekhitalifiana katika hukumu za kuzifanyia kazi Hadiyth za aina hii katika makundi matatu:

 

 

1-Wapo wanaosema kuwa Hadiyth hizi hazifai kuzifanyia kazi kabisa, yote sawa iwe katika kuamrisha mambo ya Fadhila au katika Hukmu. Na hii ni kauli ya Yahyay bin Ma'iyn na Abu Bakr bin Al-'Arabiy na pia Al-Bukhaariy na Muslim.

 

 

2-Wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi.

 

 

3-Na wengine wakasema kuwa Hadiyth hizi zinaweza kufanyiwa kazi katika mambo ya Fadhila na katika kuwaidh watu tu. Na kwamba zisitumike katika kutoa hukmu au katika ‘ibaadah, tena ziwe zimekamilisha baadhi ya masharti kama vile asituhumiwe mmojawapo wa wapokezi wake kwa uongo au ufasiki n.k. Na pia udhaifu wa Hadiyth usiwe mkubwa sana, na pia mtu anapoelezea Hadiyth ya aina hii awajulishe watu kuwa ina udhaifu ndani yake. 

 

Anasema Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj Al-Khatwiyb katika kitabu chake ‘Al-Mukhtaswar Al-Wajiyz fiy 'Uluwm Al-Hadiyth:

“Mimi naunga mkono rai ya mwanzo inayosema kuwa Hadiyth dhaifu zisifanyiwe kazi kabisa. Zipo Hadiyth za kutosha zilizo Swahiyh katika mambo ya Fadhila na mawaidha kiasi ambapo haina haja ya kuingiza Hadiyth zenye shaka zinazoweza kuwa ni maneno ya uongo aliyozuliwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

   

Pia Fadhila na Tabia njema ni katika mambo muhimu sana katika Dini kwa hivyo haina haja kuzitumia Hadiyth dhaifu kwa ajili yake.”

 

Rai ya Dr. Muhammad Al-‘Ajjaaj ni bora zaidi kwa sababu mtu atawezaje kuiamini Hadiyth iliyosimuliwa na Mudallis, mtu mwenye kubadilisha majina ya Mashaykh au ya miji akijua kuwa anawadanganya wasikilizaji wake, au muongo ‘Kadhaab’ anayependa kuwadanganya watu katika mambo ya kidunia ambaye hatoshindwa kuwadanganya katika mambo ya Ddini.

 

Na vipi mtu ataweza kuifanyia kazi Hadiyth Mudhtwarib inayogongana na Hadiyth Swahiyh au Hadiyth Matruwk iliyodhoofishwa kwa ajili ya tabia ovu za msimulizi kwa ajili ya uongo na ufasiki n.k.

 

 

Na Allah Anajua zaidi

Elimu Ya Hadiyth: Maana Ya Idadi Fulani Ya Imaam Wa Hadiyth

 Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na As-Sab’ah (watu saba), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:

 

1- Al-Bukhaariy

2- Muslim

3- At-Tirmidhiy

4- An-Nasaaiy

5- Abuu Daawuwd

6- Ibn Maajah

7- Ahmad

 

 

 

 

Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na As-Sittah (watu sita), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:

 

 

1-Al-Bukhaariy

2-Muslim

3-At-Tirmidhiy

4-An-Nasaaiy

5-Abuu Daawuwd

6- Ibn Maajah

 

 

 

Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Al-Khamsah (watu watano) basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:

 

1- At-Tirmidhiy

2- An-Nasaaiy

3-Abuu Daawuwd

4- Ibn Maajah

5- Ahmad

 

 

 

Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Al-Arba’ah (watu wanne), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:

 

1- At-Tirmidhiy

2- An-Nasaaiy

3- Abuu Daawuwd

4- Ibn Maajah

 

 

 

 

Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Ath-Thalaathah (watu watatu), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:

 

1- At-Tirmidhiy

2- An-Nasaaiy

3-Abuu Daawuwd

 

 

 

Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Ash-Shaykhaan (Mashaykh wawili) au Asw-Swahiyhayn (Swahiyh Mbili) au Muttafaqun 'alayhi (Wameafikiana juu yake), basi wanaokusudiwa hapo ni:

 

1- Al-Bukhaariy

2- Muslim

Historia Fupi Ya Imaam Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (رحمه الله)

Jina Lake:

 

Ahmad bin ‘Aliy bin Muhammad, bin Muhammad, bin ‘Aliy, bin Mahmuwd, bin Ahmad, bin Ahmad bin Al-Kinaaniy Al-‘Asqalaaniy. Umaarufu wake ni Ibn Hajar ‘Asqalaaniy.

 

 

Babu zake waliishi Asqalaan ambapo walifika huko katika mwaka wa 583H. Jiji la Asqalaan liko Palestina huko Gaza. Neno Hajar ni jina la mmoja wa babu zake. Kun-ya yake ni Abul-Fadhwl na Laqab yake ni Shihaabuddiyn.

 

 

Kuzaliwa Kwake:

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) alizaliwa tarehe 12 mwezi wa Sha'baan, 773H. Inasemekana pia amezaliwa tarehe 10 Sha’baan.  Alizaliwa Misri karibu na  ufukoni wa mto wa Nile alikulia huko huko.    

 

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alikuwa yatima. Baba yake ambaye alikuwa Mwanazuoni mkubwa na mfanya biashara alifariki katika mwaka wa 777H akimwacha Ibn Hajar (Rahimahu-Allaah) akiwa na miaka minne tu. Mama yake alifariki kabla ya hapo na kwa hivyo alikuwa yatima kutoka kwa wazazi wake wote wawili.

 

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) amekulia katika familia yenye maadili mema na wazazi wenye ‘ilmu na wenye kushajishana katika kutafuta ‘ilmu.

 

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alikuwa ana kaka mkubwa ambaye alikuwa ni ‘Aalim, lakini alifariki kabla ya Ibn Hajar,  na kwa sababu hii, baba yake alikuwa na majonzi makubwa na huzuni mno.  Mmoja wa Swaalihiyna Shaykh Yahyaa Asw-Swaanifiriy aliota ndoto akambashiria baba yake Ibn Hajar akamwambia kwamba atarithiwa (‘ilmu yake) na mtu ambaye atakuwa bora kuliko yeye, atakayekuwa na maisha marefu na kwamba atatoka katika mgongo wake ‘Aalim atakayejaza dunia kwa ‘ilmu.  Ibn Hajar   ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) mwenyewe kisha akasema:  "Nilizaliwa kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akanifungulia mikono.” Kwa maana: Allaah Amemjaalia nuru ya 'ilmu kubwa na akili nzuri ya busara.

 

 

Ibn Hajar  ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alilelewa na Zaakiy Al-Kharuwbiy ambaye alikuwa tajiri mfanya biashara maarufu.  

 

 

Ibn Hajar  ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) anahesabiwa kuwa ni mmoja wa watu adimu katika Historia ya Kiislamu. Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah) alisema: "Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alikuwa miongoni mwa ‘Ulamaa wakubwa kabisa, ambaye alihifadhi   Hadiyth kwa usahihi kabisa wa hali ya juu.”

 

 

Elimu Yake:

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alianza madrasa akiwa na umri wa miaka mitano, akahifadhi Qur-aan akiwa na umri wa miaka tisa. Alikuwa na akili nzuri mno ya kuhifadhi; aliweza kuhifahdi Suwraah Maryam kwa siku moja tu.

 

 

Mlezi wake; Zaakiy Al-Kharuwbiy alikwenda naye Hajj, akabakia huko na alipofika umri wa miaka kumi na mbili aliimamisha Waislamu Swalaah za Taraawiyh katika Masjid Al-Haram Makkah. Alikuwa ni mtoto tofuati na wenzake kutokana na upeo wa ‘ilmu yake na kuhifadhi kwake Qur-aan na kuweza kuimamisha watu katika umri mdogo kama huo. Hapakuweko na mtoto ambaye aliyelingana sawa naye katika ‘ilmu. Alipokuwa Makkah alihudhuria duruws za ‘Ulamaa waliokuwa wakifundisha huko.

 

 

Mnamo mwaka wa 786H Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alihama kutoka Makkah kurudi Misr ambako alihifadhi vitabu kadhaa vya mukhtasari  mfano: ‘Umdatul-Ahkaam cha Al-Maqdisiyy na Al-Haawiy ambacho ni cha  Fiqh ya Ash-Shaafi’iy na pia  Al-Mukhtasar Al-Haajib ambacho ni cha Usuwl Al-Fiqh, na vitabu vingine vya sarufi ya lugha ya Kiarabu.

 

 

Alipofika umri wa miaka kumi na tisa aliisoma Qur-aan yote kwa Tajwiyd mbele ya Shihaab Al-Khayuwtwiy na alizisoma Hadiyth za Swahiyh Al-Bukhaariy mbele ya Mashaykh mbali mbali .

 

 

 

Akazidi kutafuta ‘ilmu katika sayansi mbalimbali, kama Tafsiyr na Qiraa-ah.  Alikuwa akipenda sana kusoma Historia. Na alipenda sana kusoma fasihi ya lugha ya Kiarabu. Mmoja wa ‘Ulamaa   Al-Badr Al-Bushtakiy alimhimiza kusoma Al-Ghaaniy, ambayo ni vitabu vikubwa vilivyoandikwa katika fasihi ya Kiarabu. Vitabu hivyo vilikuwa ni mjeledi  takriban ishirini mpaka thelathini na Ibn Hajar (Rahimahu-Allaah) alivisoma vyote kwa umakinifu hadi akawa, pindi akisikia shairi aliweza kutambua mtunzi wake na kufahamu kwa kina shairi hilo.  Alipokaribia kufikia umri wa miaka ishirini na tano alikuwa ameshachuma na kukusanya ‘ilmu ambayo hapakuweko mtu aliyeweza kukusanya ‘ilmu kama yeye.  

 

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) aliandika mashairi mwenyewe. Akaanza kusoma zaidi Sayansi ya Hadiyth na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamjaalia mapenzi ya Hadiyth yakamsukuma kujifunza Sayansi ya Hadiyth kuzihifadhi moyoni mwake.   

 

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) akazidi kupatwa  shauku kubwa na bidii ya kuzidi kutafuta elimu. Aliweza kujifunza elimu kubwa na alibarikiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)mkatika fani hiyo. Alikuwa akitembea sana masafa na safari  za asubuhi na jioni kutafuta ‘ilmu kutoka kwa ‘Ulamaa wa zama zake.

 

 

Alisafiri kwenda Hijaz Sham, Syria, Misri akifika mpaka Alexandria, na sehemu zingine pia, ambapo aliweza kuchuma faida tele ya ‘ilmu na pia akanufaisha watu kwa ‘ilmu.

 

Alisafiri pia kwenda Yemen ambako alikutana na  baadhi ya ‘Ulamaa  kama Fayruwz Aabaadiy  ambaye ni ‘Aalim bingwa mkubwa wa sarufi ya Kiarabu ambaye aliandika moja ya kamusi ya Lugha ya Kiarabu inayojulikana kama Qamuws Al-Muhiytw. 

 

 

Pindi Ibn Hajar  ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alipokuwa na umri wa miaka sitini na kipindi hiki alikuwa tayari ni ‘Aalim mkubwa,  lakini hii haikumzuia kusafiri kwa ajili ya  kutafuta ‘ilmu.  Hii inaonyesha  jinsi gani Imaam huyu mkubwa alivyokuwa na shauku na kuthibitika kwake kutafuta ‘ilmu kutoka kwa ‘Ulamaa wengineo. 

 

 

Daraja Yake ‘Ilmu Na Hadhi Yake:

 

‘Ulamaa wa zama zake walimpa  Ibn Hajar  ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) kipaumbele na walimheshimu na akaheshimika katika zama zake na zama za baada yake. 

 

Al-Buqaa'iy alisema kumhusu Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) kwamba: “Yeye ni Imaam wa Waislaam.”  

 

Ash-Shawkaaniy amesema: “Yeye ni Al-Haafidhw Maarufu mwenye upeo wa ‘ilmu ya Hadiyth.”

 

Basi ilikuwa anapotajwa mtu kwa “Al-Haafidhw” ilijulikana moja kwa moja kuwa ni Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah)

 

 

Kufundisha Kwake:

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alifundisha Sayansi tofauti za Kiislam kama Tafsiyr ya Qur-aan, Qiraa-ah, Hadiyth, Fiqh (Shariy’ah) na kadhaalika. Alikuwa Mufti pia, hivyo alitowa Fatawa kwa watu.  Alijishughulisha sana kuendeleza ‘ilmu  ya Hadiyth,  akiifundisha na akiiandika. Alitoa mawaidha mahali pengi kama Al-Azhar, Jami’ ‘Amr, na penginepo. Pia alikuwa akifundisha wanafunzi wake kwa imla kutoka katika hifdhw yake. ‘Ulamaa wengineo, Qadhi na Mufti walikuwa wakisafiri kwenda kwake kuchota elimu yake.  

 

 

Walimu Wake Wengineo:

 

Miongoni mwa ‘Ulamaa  mashuhuri ambao alijifunza kutoka kwao alikuwa Al-Hafidhw Al-Iraqi na Ibn Al-Mulaqqin, ambao walikuwa ‘Ulamaa wawili mashuhuri wa Hadiyth na alijifunza kutoka kwa ‘Ulamaa hawa  wawili na ‘Ulamaa wengine kama wao.  Aliishi pamoja na Az-Zayn Al-Iraqi kwa miaka kumi. Pia alisomeshwa na Al-Balqini, Ibn Al-Mulaqqin,   Alijifunza Kiarabu kutoka kwa Al-‘Amari, alijifunza ufasaha wa lugha na mashairi kutoka kwa Al-Badr Al-Mushtaki, na alijifunza uandishi utoka kwa baadhi ya ‘Ulamaa. Pia alikuwa akiisoma Qur-aan katika Viraa vyote saba kutokwa kwa At-Tanuwkhiy.

 

 

Kazi Zake:

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) aliandika vitabu vingi vinavyopindukia mia moja na khamsini; vingi kati ya hivyo vilikuwa ni fani ya Hadiyth.   Wafalme na wana wafalme wakawa wanapeana zawadi ya vitabu vyake.

 

Kitabu chake maarufu ni Fat-h Al-Baariy ambacho ni Sharh ya Swahiyh Al-Bukhaariy.  Kitabu hiki hakika kilihesabika kuwa ni Kamusi ya Sunnah, bali ni Kamusi ya Sayansi za Kiislaam. 

 

Kitabu hiki kilihesabiwa kuwa na faida kubwa kwa kuwa ilikuwa inapoulizwa maswali, basi Ibn Hajar (Rahimahu-Allaah) alitoa majibu kutokana na Kitabu hiki na kuwafanya waulizaji wapate fahamu kamili ya maswali yao. 

 

Pia katika kazi zake nyenginezo ni Tahdhiyb At-Tahdhiyb, Taqriyb At-Tahdhiyb, Lisaan Al-Miyzaan, Al-Iyswaabah fiy Tamyiyz Asw-Swahaabah, na Buluwgh Al-Maraam Min Adillat Al-Ahkaam.

 

Pia kazi zake (Vitabu) vingi mno mbalimbali vya Sayansi za Hadiyth, Tafsiyr, Uluwmul-Qur-aan.

 

 

Wadhifa:

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alikuwa Ustaadh, Mwandishi, Mufti na Qadhi wa Misri, kisha Sham, ikaongezewa kwenye eneo la madaraka yake, ambayo aliyashikilia kwa zaidi ya miaka ishirini. Mara ya kwanza, alikataa kukalia kiti cha Uqadhi, mpaka pale Sultani alipompelekea shauri moja makhsusi. Kisha akakubali kumwakilisha Al-Balqini alipomuomba sana awe Qadhi. Tena akashika wadhifa kwa ajili ya watu wengine mpaka alipoteuliwa akalie kiti cha Uqadhi Mkuu. Kisha akaondoka, lakini akalazimika kushika wadhifa wa Uqadhi mara saba, hadi alipoacha karibu na mwaka wa kufariki kwake

 

 

Khulqa (Tabia) Zake:

 

Kuhusu khulqa zake, Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alikuwa mnyenyekevu mno hadi kwamba alipoulizwa: “Je umepata kukutana au kumjua mtu kama wewe?” Alijibu:

 

فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾

Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa. [An-Najm: 32]

 

Na baadhi ya Swahibu zake walimuuliza: “Je wewe umehifadhi zaidi au Adh-Dhahabiy?” Alinyamaza kimya bila kujibu lolote.

 

Kwa hiyo, hakuwa mwenye kujigamba kutokana na ‘ilmu yake wala daraja yake katika jamii.

 

Alikuwa pia mvumilivu, na mwenye subira na ustahamilivu mkubwa sana, mwenye zuhd (kuipa mgongo dunia). Ilisemwa kuwa alikuwa mcheshi, mwaminifu, mwerevu, mtu anaejinyima anasa, asiyejiweka mbele mbele, mkarimu, mtoa swadaqah, na aliyedumu katika Swalaah na Swiyaam za faradhi na za Sunnah. Hakuwacha kamwe Swalaah za jamaa wala hakupata kuacha kuamka kuswali usiku hadi alipofika kupata maradhi yake aliyofia.  Imesemekana kwamba alikuwa akifunga Swiyaam siku moja na ya pili yake akila.

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) alikuwa akila chakuka kidogo tu. Alikuwa mwangalifu katika kula chakula cha watu wengine, hakuwa na makuu, na alipokuwa safarini alikuwa akila chochote anachokipata. Pindi alipoishiwa na pesa za kununulia chakula, alikuwa akila chakula duni;  chakula ambacho  watu wa kawaida hawangeweza kula.   Alikuwa anatahadhari na kukhofia sana kula chakula cha watu kutokana na chumo la haraam.      

 

Alikuwa na khulqa na desturi nzuri ya kuwasiliana na Imaam, wawe ni wa daraja la juu au watu duni kabisa, na akitaamuli vizuri na watu alioishi nao, wawe wazee au vijana, maskini na mafakiri.

 

Kwa ujumla Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alikuwa na akhlaaq njema za kila aina, akhlaaq ambazo apasavyo kuwa nazo Muumini wa kweli. As-Sakhaawiy aliandika mlango mzima kuhusu akhlaaq za Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah)

 

 

Kufariki Kwake:

 

 

Ibn Hajar ‘Asqalaaniy (Rahimahu-Allaah) alianza kuumwa katika mwezi wa Dhul-Qa’dah mwaka 852H lakini hakuacha kufundisha wala kuacha kazi zake nyenginezo za kunufaisha Waislamu katika mambo ya dunia yao na Aakhirah yao, wala  hakuacha Swalaah ya jamaa. Kisha maradhi yakamzidi katika mwezi wa Dhul-Hijjah akashindwa kuhudhuria Swalaah ya ‘Iydul-Adhwhaa, ila aliswali Swaaah ya jamaa usiku wa kabla yake. Kisha ilipofika Jumanne tarehe 14 Dhul-Hijjah akazidiwa mno na maradhi hadi kufika Jumamosi tarehe 18 Dhul-Hijjah akafariki baada ya Swalaah ya ‘Ishaa.

 

 

Inasemekana kuwa aliswaliwa Swalaah ya Janaazah na Khaliyfah wa Al-‘Aabasiyy au Qaadhi  mkuu al-Baqlaaniy. Mazishi yake Misr yalihudhuria na umati wa Waislamu akiwemo   Sultan, pamoja na viongovi wengineo wa Kiislamu na ‘Ulamaa wakubwa na watu wengi mno walihudhuria hadi ilisemekana kwamba idadi ya watu waliohudhuria walifikia maelfu.  Na akaswaliwa pia Swalaatul-ghayb (Swalaah ya ghaibu) sehemu kadhaa za Kiislamu ikiwemo Makkah, Sham, na miji mingineyo ya  Kisalaam. Siku ya kufariki kwake ilikuwa siku adhimu ya huzuni kubwa kwa Waislamu.

 

Allaah Amrehemu Alimpe malipo mema ya Jannatul-Firdaws kwa juhudi zake katika Uislaam na kunufaisha kwake Waislamu.

 

 

Nguzo za Uislamu

Shahadah

لآ اِلَهَ اِلّا اللّهُ مُحَمَّدٌ رَسُوُل اللّهِ

hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah

Swalaah

kusimamisha Swalaah

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 5]

swawm Ramadhwaan.

kufunga swawm Ramadhwaan.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾ Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 183]

Zaka

kutoa Zaka

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ} النور:56} "Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mtume, ili mpate kurehemewa." (Suratu An-Nur: 56),

Hajj

kuhiji Al-Bayt (Makkah)

“’Umrah mpaka ‘Umrah ni kafara ya madhambi yatendwayo baina yake. Hajjun-Mabruwr (Hijjah iliyokubaliwa) haina malipo isipokuwa Jannah.”[1] [Al-Bukhaariy, Muslim]

Maps And Contact

Je' unamaoni au ushauri kuhusiana na Tovuti hii wasiliana nasi hapa chini.

wasiliana nasi

Name

Email *

Message *


how to add google map in wordpress